Monday, October 26, 2015

Anonymous

MATOKEO RASMI Ya Wabunge na Madiwani Katika Majimbo Mbalimbali Ambayo Yameshatolewa

Update: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.
Update: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini na Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.

Update:
Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.
Update: Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini

Jimbo la Serengeti
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe

Jimbo la Chalinze

Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470

Jimbo la Moshi Mjini

Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920

Jimbo la Bunda Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.
Jimbo la Peramiho

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Jimbo La Arumeru Mashariki

Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo
Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847

Jimbo la Shinyanga

Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi

Jimbo la Tandahimba

Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088

Jimbo la Mkinga

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mkinga Dustan Kitandula ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Mbinga Mjini

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge:
Vicent Nyerere(Chadema) 25,549 na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836.

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Mbinga Vijijini

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Monduli

Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Aggrey Mwanry
Jimbo la Siha

Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).

Jimbo la Tunduma

Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

Jimbo Buyungu
Ubunge:
Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.

Christopher Chiza

Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo

Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge:
Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.
Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo

Jimbo la Lindi Mjini

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Endelea kufuatilia hapa kandiliyetu.com kwa updates zote muhimu za uchaguzi mkuu na matukio mbalimbali kama bado hauja-like page yetu ya facebook bonyeza hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.