Musa Mateja
USIPIME! Mapokezi ya ‘kichaa’ wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipotua jijini Dar, juzi na tuzo
tano alizojitwalia nchini Marekani yamesababisha mafuriko ya watu na
kufungwa kwa baadhi ya barabara na shughuli kusimama, Risasi Jumamosi
lilikuwa kwenye msafara.
TUANZIE UWANJA WA NDEGE
Ilikuwa mishale ya saa 8:00 mchana
ambapo mashabiki wengi walikuwa wakimsubiri nje ya Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA) kabla ya kutokea akiwa
amezishika tuzo zake hizo tano.
Baadhi ya mashabiki wa nyota huyo, wakiwemo bodaboda kibao, walisababisha mshangao mkubwa uwanjani hapo kutokana na idadi yao huku wakiimba; ‘rais…rais…rais wetu Diamond’. Wengine walikuwa na mabango ya kumsifia na mengine ya kuwakejeli wapinzani wake.
Baadhi ya mashabiki wa nyota huyo, wakiwemo bodaboda kibao, walisababisha mshangao mkubwa uwanjani hapo kutokana na idadi yao huku wakiimba; ‘rais…rais…rais wetu Diamond’. Wengine walikuwa na mabango ya kumsifia na mengine ya kuwakejeli wapinzani wake.
MAFURIKO KAMA LOWASSA, MAGUFULI
Mwingine alisema: “Huu kweli ni mwaka wa tofauti, eti hata Diamond naye ana mafuriko! Mimi nilijua ni Lowassa (Edward) na Magufuli (John) tu.”
Baada ya kusalimiana na mashabiki wake
kisha mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’, uongozi wake wa Wasafi Classic
Baby (WCB) na ndugu zake wengine, Diamond alizungumza na vyombo vya
habari akishukuru mashabiki kwa kumpa sapoti hadi akanyakua tuzo hizo.
Baada ya kuona msongamano mkubwa,
Diamond aliamrishwa na mashabiki wake atembee ambapo alitii kisha
wakaingia barabarani kuanza msafara.
Msafara huo ulikuwa ukielekea kwenye
Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kupitia Barabara ya
Nyerere kabla ya kuzuiliwa na askari waliomwamuru apande kwenye gari ili
kuepusha msongamano
Baada ya kutii agizo hilo, Diamond aliendelea na msafara wake kupitia
Barabara za Mandela, Uhuru, Lumumba, Morogoro, Kawawa kisha msafara
ulikata kushoto kuelekea nyumbani kwao, Tandale.
Baada ya Tandale, alielekea Escape One
ambapo alizungumza tena na wanahabari kisha kupiga picha na mashabiki
wake akiwa na tuzo hizo.Kwenye barabara hizo zote kulikuwa na mafuriko
kiasi cha baadhi ya watu kuuliza ni mgombea gani anayefanya kampeni
barabarani muda huo!
Ndani ya Escape One, mashabiki
waliendelea kusherehekea ushindi wa Diamond kwa kunywa, kula na
kuserebuka na muziki hadi muda mbovu.
TUZO NYINGINE YANUKIA
Akiwa Escape One, Diamond alisema kuwa kuna tuzo nyingine inanukia ya
MTV Europe Music ambapo alipigiwa simu na kuelezwa kwamba ameteuliwa
kushiriki akiwa msanii pekee kutoka barani Afrika zitakazofanyika jijini
Milani, Italia, Oktoba 28, mwaka huu.
Kufuatia siku kubaki chache, Diamond
aliwaomba mashabiki wake wampigie kura kwa wingi ili achukue tuzo hiyo
muhimu itakayomkutanisha na mastaa wengi wakubwa duniani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.