Nyumba ya Diamond inayodaiwa si yake.
GLADNESS MALLYA IMELDA MTEMA
IMEVUJA! Ile nyumba ya kifahari
iliyoaminika ni ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
imefahamika kuwa siyo yake kama wengi walivyokuwa wakifahamu.
Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na
maneno ya wambeya yaliyokuwa yakielekezwa kwa mama mzazi wa staa huyo,
Sanura Kasimu ‘Sandra’ mitandaoni kwamba kwa nini asiondoke kwenye
nyumba hiyo na kumuacha mwanaye awe huru ndipo mwanahabari wetu
alipomtafuta mama Diamond na kumuuliza kuhusu maoni ya wambeya hao, bi.
mkubwa huyo akasema hawezi kuondoka kwani nyumba hiyo siyo ya Diamond
bali ni mali yake.
“Kwa taarifa yenu hii nyumba ni ya
kwangu na makaratasi yote yameandikwa jina langu hao wanaosema nimwache
Nasibu awe huru hawajui lolote, mimi ndiyo nimesimamia kila kitu na
Nasibu hakuwahi kusimamia hata siku moja, hii ni nyumba yangu.
“Wanaosema awafukuze ndugu zake
nawaambia kwamba hapa hakuna mtu atakayetoka, mwanangu nimeteseka naye
hakuna anayejua tumetokea kwenye maisha gani kwa hiyo naomba watu waache
kuchonga sana,” alisema mama Diamond.
Note: Only a member of this blog may post a comment.