Uchumba wa
mastaa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma na Bond Bin Suleiman ambao
ulikuwa umepamba moto huku hivi karibuni ikidaiwa wataoana baada ya
uchaguzi, umevunjika baada ya Wastara kusalitiwa.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya
jina lake kilidai kuwa, wawili hao walikuwa wakienda vizuri lakini hivi
karibuni Bond alibainika kumsaliti mwezake kwa kuwa na mwanamke mwingine
aliyezaa naye.
“Uchumba wao ulikuwa unaenda vizuri tu
lakini mara kwa mara Bond amekuwa akimliza mwenzake kwa kuchepuka.
Wastara akawa anaziba masikio kwa kuwa anampenda.
“Kuna wakati Bond alidaiwa kumpa mimba
mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grace, Wastara akafunika, sasa naona
amechoka maana inadaiwa Bond ana mtoto mdogo aliyezaa na mwanamke
mwingine.
Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati
la gazeti hili, mwandishi wetu alimwendea hewani Wastara ambaye alikiri
kusikia habari za Bond kuwa na mtoto ila akasema anafuatilia na akijua
ukweli atalazimika kujiweka pembeni.
“Mh! Kama hizo habari na nyinyi
zimewafikia basi, maana mimi nilizisikia kijuu juu nikaona nitazifanyia
kazi ila kiukweli kama ni hivyo, najiweka pembeni. Nimekuwa nikimpigia
simu lakini simpati kwa takriban wiki nzima sasa, sijui shida iko wapi,”
alisema Wastara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.