HALIMA Yahya ‘Davina’
amehamasika na mambo ya kisiasa hivyo, kujiandaa kwa kujifua vyema kwa
ajili ya msimu ujao wa uchaguzi (2020).
Akizungumza na paparazi wetu hivi
karibuni, Davina ambaye ni msanii wa filamu Bongo, alisema kufuatia
kupata fursa ya kushiriki kampeni kwa nafasi yake, maeneo mbalimbali ya
nchi, amejikuta akishawishika kuwa kiongozi na kwamba baada ya miaka
mitano, endapo Mungu atamjaalia uzima, atagombea nafasi ya ubunge,
mkoani Iringa.
“Sikuwa na mzuka na mambo ya siasa
kabisa lakini kushiriki kwangu kampeni za kumnadi Magufuli maeneo
mbalimbali nchini, nimeingiwa na ujasiri wa kujiingiza huko na naamini
nitamudu nikijipanga, kikubwa tuombe uzima,” alisema Davina.

Note: Only a member of this blog may post a comment.