Najua kuna watu mtakuwa mnataka kufahamu
kwamba, Je kama mtu aliyejiandikisha Dar es Salaam na yupo Arusha
kikazi atafanye? ,majibu yako hapa yamejibiwa na Mkurugenzi wa huduma za
kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe.
‘Mtu atapigia kura mahali
ulipojiandikisha kama ulijiandikisha Dar es Salaam hakikisha unarudi
kuja kupigia kura Dar es Salaam kwa hiyo hatoruhusiwa mtu kwa mujibu wa
sheria kupigia kura sehemu yoyote kifungu cha 91 kifungu kidogo cha
tatu A kinasema mtu ataenda sehemu ya kujiandisha na kuruhusiwa kupiga
kura’ – Emmanuel Kawishe
‘Kwa hiyo kama mtu akiwa Dar es Salaam
labda amejiandikisha Arusha anachotakiwa ni kufanya maamuzi ya kwenda
Arusha kwenda kituo alichojiandikisha ndipo aweze kushiriki kupiga kura’
– Emmanuel Kawishe
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe.

Note: Only a member of this blog may post a comment.