Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Dar Es Salaam Young African Danny Mrwanda kwa sasa yupo katika klabu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa inayoshiriki Ligi daraja la kwanza. Mrwanda ambaye amemalizana na Yanga mwishoni mwa msimu uliyopita alijiunga na Lipuli FC ya Iringa baada ya kutaka kuwa huru.
Wengi walikuwa wanataka kufahamu ni nini kilichomfanya Danny Mrwanda kwenda kucheza Lipuli FC
ya daraja la kwanza ni kweli anaelekea kustaafu soka? uwezo wake
umeisha? amekosa klabu yoyote ya Ligi Kuu inayomuhitaji katika Ligi Kuu Tanzania bara, millardayo.com ilimtafuta kutaka kufahamu hilo. Majibu yake yalikuwa haya.
“Kwanza
uelewe ningetaka kucheza Ligi Kuu Tanzania nisingeshindwa kucheza
katika timu yoyote, kuna timu nyingi tu zilikuwa zinanihitaji. Lipuli
mimi nimekwenda kwa sababu maalum sitaki nibanwe kwa kipindi hiki kwani
wakati wowote naondoka, mimi nipo Lipuli kama sehemu ya mazoezi ili muda
wangu ukifika wa kuondoka, naondoka nikiwa katika kiwango kizuri, kwani
muda wowote kuanzia hivi sasa naenda Malaysia”>>> Danny Mrwanda
Mrwanda amewahi kutamba katika vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Tanzania bara kabla ya kuamua kwenda kujikita katika Ligi Kuu Vietnam kwa zaidi ya miaka 4. Kwa sasa Danny Mrwanda ambaye awali kulikuwa na stori kuwa anaenda Thailand, amethibitisha kuwa na mipango ya kwenda kucheza soka katika Ligi Kuu Malaysia muda wowote kuanzia hivi sasa.
Hii ni sauti ya Danny Mrwanda mtu wangu
Note: Only a member of this blog may post a comment.