Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema hayo jana na kuongeza kuwa hali hiyo inaweza kuchochea uvunjifu wa amani.
Alisema wagombea hao wamekuwa wakikiuka taratibu na sheria za nchi wakati wakifanya kampeni.
“Nawakumbusha wagombea na wafuasi wao kwamba kabla ya kampeni kuanza vyama vya siasa vilisaini vitabu vya maadili ya uchaguzi.
“Na kwamba hawaruhusiwi kufanya mambo ambayo hayapo kisheria, atakayekiuka ataadhibiwa,” alisema Kamanda Mwaibambe.
Pia, alisema wagombea na wafuasi wao hawaruhusiwi kutumia vipaza sauti kuanzia saa 12 jioni ili kuepuka kukiuka taratibu na maadili ya uchaguzi.
Hata hivyo, Kamanda Mwaibambe alisema kuanzia sasa polisi hawatamvumilia mtu atakayevunja taratibu na sheria katika kipindi kifupi kilichobaki cha kampeni hadi itakapofikia siku ya uchaguzi.
Note: Only a member of this blog may post a comment.