Mtoa taarifa ambaye ni mtangazaji wa ITV anasema, mmiliki wa kituo hicho Reginald Mengi baada ya kulalamikiwa na Lowassa juu ya video hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, alitaka wote waliohusika kwenye utayarishaji wake wawajibike.
Anasema uandaaji wa matangazo hayo ya Lowassa ambayo yameanza kurushwa na ITV, yalichukua muda mrefu kuyaandaa ambapo Lowassa kutokana na hali yake ilimlazimu kurudia kila mara na wakati mwingine alionekana kushindwa kuongea na kukohoa sana.
Mtoa taarifa anasema tayari baadhi ya watendaji wamesimamishwa kazi kwa kitendo cha kusambaza video zinazomdhalilisha Lowassa na kuonyesha udhaifu wake ambao Chadema wanajitahidi kuuficha.
Chanzo: By Naface Kutoka : Jamii Forums


Note: Only a member of this blog may post a comment.