Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ZEC kutangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar October 28 2015, Kiongozi wa zamani wa chama cha CUF, Professor Ibrahim Haruna Lipumba na mgombea Urais wa Zanzibar kwa mwamvuli wa CUF na Umoja wa vyama vya UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad wamezungumzia kuhusu kuchukuliwa kwa hatua hiyo.
“Nimeshtushwa
na hatua hiyo hasa ukizingatia Uchaguzi umefanyika tarehe 25 leo ni
tarehe 28, na sababu ambazo Mwenyekiti amezitoa ni mambo ambayo
yangeweza kujulikana mapema sana… Tume ya Uchaguzi ya Taifa ambayo
inatangaza matokeo ua Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa
inatangaza Kura za matokeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ambazo
zimefanyika kwenye uchaguzi huohuo mmoja na Tume haijasema kwamba
uchaguzi ule ulikuwa mbovu.”- Professor Ibrahim Haruna Lipumba.
“Hata
watazamaji wa Kimataifa wamesema utaratibu wa kupiga Kura na kuhesabu
vituoni ulikwenda vizuri… nashukuru viongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad amewaomba Wazanzibar kuwa watulivu wakati suala hili
linashughulikiwa.” >>> Prof. Lipumba.
“Ilipaswa
iundwe Tume ya Majaji watazame tamko alilolitoa lina uhalali gani,
wazungumze pia na Wajumbe wa Tume ya uchaguzi kwa sababu tamko hilo
limevunja Sheria halina uhalali wa kisheria.”
Hili ndio jibu la Professor Lipumba kuhusu anayeweza kumaliza tatizo lililotokea Zanzibar >>> “Mtu
ambaye ana uwezo na wajibu mkubwa kwenye hili ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kwa sababu yeye ni Rais na Mwenyekiti wa CCM,
ashauriane na Rais wa Zanzibar ili akubali kuunda Serikali ya kitaifa,
imefika wakati Dk. Shein aoneshe ukomavu wa kisiasa.”
“Kuna
watu wamelalamika, nimemsikia Edward Lowassa amelalamikia matokeo ya
Uchaguzi, haya ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ameyaeleza
yanaongeza nguvu kwa Mheshimiwa Lowassa kwamba hata
Tanzania bara mambo hayakwenda sawa… Hatua aliyochukua Mwenyekiti
imevunja Sheria, isipotokea ufumbuzi mapema, patatokea vurugu.” >>> Professor Ibrahim Haruna Lipumba.
HAPA NAANZA NA KILE ALICHOKISEMA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
“Chama
cha CUF kimepata taarifa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar
ametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu bila kuwashirikisha
Makamishna wenzake wa Tume ya Uchaguzi…. CUF imeshtushwa na taarifa hii
ambayo iko kuinyume na Sheria za uchaguzi ya Zanzibar, Mwenyekiti hana
mamlaka ya kufuta Uchaguzi huo.” >>> Maalim Seif Sharif Hamad.
“Mwenyekiti
hakutafakari kwamba kuufuta uchaguzi Zanzibar kunaathiri pia Uchaguzi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wapiga Kura ni walewale
waliomo kwenye daftari la wapiga Kura wa ZEC.” >>
“Rais
wa Jamhuri ya Muungano hawezi kupatikana kwa kupigiwa Kura na wananchi
wa Tanzania bara pekeyake… Tunatambua kwamba hatua hii imekuja baada ya
majaribio ya kulazimisha ushindi kushindikana.”
“CUF
hatutambui uamuzi huo wa Mwenyekiti wa Tume ya ZEC, tunaitaka Serikali
na CCM kuiacha Tume iendelee na uhakiki wa matokeo na itangaze mshindi… Tunatoa wito na kuomba Wazanzibar kwa ujumla kubaki watulivu..” >>> Seif Sharif Hamad.
Sauti yote ya Maalim Seif Sharif Hamad hii hapa kama umepitwa na hii taarifa.
Hapa ni sauti ya Professor Ibrahim Lipumba
Note: Only a member of this blog may post a comment.