Klabu ya Manchester United ya Uingereza ni moja kati ya vilabu vilivyotumia fedha nyingi katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015. Toka kocha Louis van Gaal ajiunge na klabu ya Man United, uongozi wa klabu hiyo umetumia zaidi ya pound milioni 250 kwa ajili ya kusajili wachezaji.
Ed Woodward
Ed Woodward amekiri kuwa bado Manchester United itaendelea na matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake, Ed Woodward amesema Man United katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August walikuwa wakihusishwa kutaka kusajili wachezaji wengi zaidi lakini walifanikiwa kusajili sita. Hivyo Man United bado itaendelea kutumia fedha nyingi katika usajili ili kuimarisha kikosi.
Note: Only a member of this blog may post a comment.