Friday, October 23, 2015

Anonymous

AJALI MBAYA Yaua Watu Zaidi ya 40 Baada ya Basi Kugongana na Lori na Yote Kuwaka Moto [+PICHAZ]

Puisseguin (1)Puisseguin (8)Ajali hiyo ilivyotokea.
Puisseguin (2)Kikosi maalum cha uokoaji kikifanya kazi yake.
Puisseguin (3)Majeruhi wakisaidiwa kupata huduma ya kwanza.Puisseguin (4) Puisseguin (5) Puisseguin (6) Ndege maalum za uokoaji.Puisseguin (7)
WATU  40 wakiwemo watalii na dereva mmoja wa lori wamefariki dunia na watano kujeruhiwa na wengine wanane kunusurika baada ya basi lao kugongana na lori na yote kuwaka moto palepale katika barabara moja Kusini Magharibi mwa Ufaransa. 

Ajali hiyo imetokea karibu na Puisseguin eneo la Gironde Mashariki mwa Bordeaux, muda mfupi baada ya basi hilo kuanza safari kutoka mji wa jirani.  Wengi wa waliokuwa kwenye basi hilo walitoka chama cha wazee kilicho katika mji wa Petit-Palais-et-Cornemps. 

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameandika kwenye Twitter kwamba serikali “imechukua hatua zote kushughulikia mkasa huo mbaya”. 

Mkasa huo ndio mbaya zaidi kutokea barabarani nchini humo tangu ajali iliyoua watu 52 iliyotokea mwaka 1982.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijabainika wakati Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls, pamoja na mawaziri wa masuala ya ndani na uchukuzi wanatarajiwa kutembelea eneo la mkasa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.