Wednesday, September 2, 2015

Anonymous

ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU WATU WANAOMTUKANA DR. SLAA


Slaa hayupo kwenye karatasi ya kura. Naona watu wanahangaika na Slaa. Wengine tuliamua kukaa kimya kwani hekima inataka hivyo. Kwa kuwa watu wameamua kumtukana Dkt. Slaa ni lazima tutoke kulinda haki yake ya kusema yake. Tutatoka na tutaungana na Slaa kuwasema walio kwenye Ballot. Slaa hayupo kwenye Ballot. Mwacheni. Jadilini hoja zake sio kumjadili yeye. Eti hata watu wasio na rekodi yeyote ya kupambana na ufisadi nchi hii leo wanainua midomo yao kumsema Slaa. Mmeanza. Tutamsaidia Slaa, tutamaliza.

Sina mapenzi na Slaa. Alihusika kuniletea shida kubwa ya kisiasa nilipokuwa napigania MISINGI. Hata hivyo naipenda zaidi Tanzania kuliko tofauti zangu na Slaa. Ni lazima aheshimiwe na alindwe. -Zitto Kabwe

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.