Imelda Mtema
Staa asiyechuja Bongo, Wema Sepetu
amefunguka kuwa hakuhudhuria kwenye 40 ya mtoto wa mwanamuziki Nasibu
Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa mpenzi wake kwa kuwa haikuwa inamuhusu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi
karibuni baada ya kumuuliza kwa nini hakuonekana kwenye sherehe hiyo,
Wema alisema asingeweza kwenda kwa kuwa haikuwa ikimuhusu hata kidogo.
“Sasa jamani ningeenda kwenye hiyo
sherehe wakati haikuwa ikinihusu kwa lolote, mfano ningeenda pale kama
nani sasa na wala sikuwa najua kama kuna kitu kama hicho kwa sababu
sikualikwa,” alisema Wema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.