Thursday, September 17, 2015

Anonymous

Warembo Wafanya Shindano la AIBU Huko Morogoro!

WAREMBO (2)
Dustan Shekidele, Morogoro
MSALA! Warembo kadhaa wenyeji wa mji wa Morogoro Ijumaa iliyopita walishiriki kufanya shindano la aibu linalodaiwa kuandaliwa na viongozi wa serikali ya mtaa na kufanyika katika Ukumbi wa Shirati, wakicheza na kutembea nusu utupu jukwaani.
WAREMBO (3)Shindano hilo maarufu kama Kanga Moko lilisababisha wananchi kukerwa na hivyo kuwaita askari, ambao hata hivyo, walishindwa kulizuia tukio hilo lililofanyika katika Mtaa wa Tupendane, Chamwino na mgeni rasmi akiwa ni kigogo wa mtaa aliyetajwa kwa jina moja la Milomo.
WAREMBO (1)Gazeti hili lilishuhudia viongozi hao wa serikali wakifurahia mabinti hao wakishindana kufanya shoo hiyo ya nusu utupu. Baada ya hapo washiriki hao walipita jukwaani wakiwa na khanga moja waliyojifunga upande mmoja huku upande wa pili wakiwa watupu,” kabla ya askari wawili kutinga ukumbini hapo, lakini viongozi wa serikali ya mtaa wakazungumza nao ‘kiutu uzima’ na kuliacha zoezi hilo likiendelea.
WAREMBO (4) 
Katika shindano hilo, Grace John aliyekuwa kinara wa kukaa kihasarahasara alishinda na kuwa Miss Shirati Khanga Part 2015 akimrithi Merry Oddo aliyetwaa taji hilo mwaka jana, Latifa Selemani alitwaa nafasi ya pili na Zamida Hemedi alishika nafasi ya tatu ambapo mgeni rasmi wa shindano hilo, Papaa Milomo alikabidhi zawadi kwa washindi hao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.