Monday, September 14, 2015

Anonymous

Ushindi wa MAYWEATHER ‘Wamboa’ Manny Pacquiao

Ushindi wa bondia Floyd Mayweather dhidi ya Andre Berto umeonekana kumboa bondia mfilipino, Many Pacquiao anaedaiwa kuwa mpinzani hatari zaidi wa bingwa huyo ambaye hajawahi kupigwa.

Manny Pacquiao na  Mayweather Jr., Baada ya Pambano lao  May 2, 2015 ,Las Vegas.
Manny Pacquiao na Mayweather Jr., Baada ya Pambano lao May 2, 2015 ,Las Vegas.
Wakati pambano la Mayweather na Berto likimalizika jana na Maywether kutangazwa mshindi, Pacquiao alipost Instagram kipande cha video kinachomuonesha akiwa anachezea piano chumbani na kuandika, “hivi ndivyo ninvyofanya nikiwa ‘bored’ (nimechoshwa kwa tafsiri isiyo rasmi).”

Pacquiao ambaye alishindwa na Mayweather katika pambano ambalo lilipewa jina la ‘pambano la karne’ huku ushindi huo ukileta utata na mvutano wa uhalali wake, aliibuka hivi karibuni na kudai kutaka marudiano na bondi hiyo Mmarekani baada ya kubainika kuwa alipewa drip za maji ya kuongeza nguvu kabla hajapanda ulingoni kupambana naye.

A video posted by Manny Pacquiao (@mannypacquiao) on
Pacquiao alimtaka Mayweather kutostaafu hadi pale watakapomaliza ubishi kwa pambano la marudiano, hoja ambayo haijapenya hata kidogo kwenye masikio ya Maywether anaekiri kuwa bondia huyo mfilipino ndiye aliyewahi kuleta upinzani mkali zaidi kwake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.