Wakati mchakamchaka wa kampeni za uchaguzi mkuu unaendelea kushika kasi huku mikutano ya wagombea urais wa CCM na Chadema ikionesha kuvuta umati mkubwa wa tu, utafiti utakaotoa picha ya mshindi unatarajiwa kuwekwa hadharani ndani ya siku 11.
“Tuko katika hatua za mwisho za kuandaa taarifa na tunatarajia kutoa matokeo ya tafiti ndani ya wiki mbili,” alisema Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Twaweza, Risha Chande.
Kwa upande wa IPSOS-Synovate, walieleza kuwa wanatarajia kutoa matokeo yao ndani ya siku chache zijazo.
Wakati taasisi hizo zikitarajia kutoa matokeo yao hivi karibuni, Mwenyekiti wa taasisi ya REDET, Dr Benson Banna alisema kuwa taasisi yake haikuweza kufanya utafiti mwaka huu kwa sababu za ukosefu wa fedha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.