MATESO! Mtoto aitwaye Chacha Robert (15),
(pichani), mkazi wa Musoma, Mara anateseka na ugonjwa wa ajabu wa kuota
magamba kama ya nyoka sehemu ya mwili hali inayomsababishia kutengwa na
jamii.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na familia yake zinaeleza kuwa,
Chacha alizaliwa hivyo na mama yake mzazi alifariki dunia saa chache
baada ya kujifungua.
“Wao kama Wakurya waliamini kwamba mama yake aliona chatu wakati akiwa mjamzito ndiyo maana mtoto akazaliwa hivyo.
“Chacha kwa sasa anasoma kidato cha kwanza kwa shida. Wanafunzi
wenzake wanamnyanyapaa na kumuoneshea vidole kila anapopita,” alisema
mtu huyo ambaye ndiye mwangalizi wa karibu wa maisha ya Chacha.
Akaendelea:
“Tulimpeleka hospitali, daktari akasema ugonjwa huo unaitwa Ichthyosis
ambao unafanana na Albinism anavyozaliwa. Na msaada anaouhitaji ni
kubadilisha nguo mara kwa mara na kula vyakula vya kiasili.
“Kwa sasa, Chacha anaishi na baba yake na babu yake na hali yao
kiuchumi si nzuri na ndiyo maana tumewaomba nyie Global mtusaidie.”
Picha kwa hisani ya Flora Show

Note: Only a member of this blog may post a comment.