Thursday, September 17, 2015

Anonymous

TUNDU LISSU Afunguka: Richmond ni ya Rais KIKWETE...Nataka Nimnyamazishe! [VIDEO]

Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu akihutubia Leo Mkutano wa kumnadi Edward Lowassa mgombea Urais wa CHADEMA (UKAWA) amesema Richmond ni ya Rais Jakaya Kikwete.
Aidha, amesema richmond sio ya mtu anayeongozana nae kwenye kampeni.

Magazeti leo yalimkariri Rais Kikwete alipokuwa Kigoma akisema mhusika wa Richmond ni yule anayeongozana na Lissu kwenye Kampeni.

Katika video hiyo,Tundu Lissu anasikika akisema maneno yafuatayo;
"Ndugu zangu wa Morogoro, Richmond ni ya Kikwete.. Richmond ni ya Kikwete narudia.. Richmond sio ya huyu anayetembea na Lissu kwenye kampeni, Richmond ni ya Kikwete. Sasa nimesema nataka nimnyamazishe. Sasa nipeni masikio yenu...." 

Nimekuwekea video hiyo hapa, bonyeza play kuicheki au download kuipakua!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.