Binadamu hupitia hatua nyingi hadi kuja kufikia mafanikio, wengi wamepata shida katika harakati za kusaka mafanikio, huenda umewahi kuwaona mastaa kadhaa wa soka wakiwa na mafanikio na hukuwahi kuwaona wakiwa katika muonekano wao wakati wapo wadogo. Ninayo list ya TBT pichaz ya mastaa wa Real Madrid.
1- Sergio Ramos beki wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, kama hufahamu Ramos ni shabiki mkubwa wa mashindano ya kupiganisha ng’ombe, mchezo ambao ni maarufu Hispania. Hizi ni TBT pichaz za beki huyo aliyezaliwa March 30 1986 Camas Hispania.
Sergio Ramos
Sergio Ramos enzi za utoto
2- Iker Casillas golikipa wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Real Madrid mwaka 1990 wakati ambao alikuwa na miaka 9, Casillas kwa sasa yupo katika klabu ya FC Porto ya Ureno. Casillas alizaliwa 20 May 1981 Móstoles Hispania baba yake José Luis Casillas alikuwa mtumishi wa kawaida wa wizara ya elimu Hispania wakati mama yake María del Carmen Fernández González alikuwa mfanyakazi wa saloon.
Iker Casillas
Iker Casillas kipindi yupo timu ya vijana ya Real Madrid
Iker Casillas kipindi yupo timu ya vijana ya Real Madrid
3- Alvaro Arbeloa beki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania ambaye amewahi kukitumikia kikosi cha Liverpool kuanzia mwaka 2007-2009. Arbeloa kazaliwa Salamanca Hispania 17 January 1983, alianza kucheza soka mwaka 2001 katika klabu ya Real Madrid na baadae akawa anacheza katika kikosi cha wachezaji wa akiba cha timu hiyo.
Alvaro Arbeloa
Alvaro Arbeloa enzi zake za utoto

Note: Only a member of this blog may post a comment.