Thursday, September 24, 2015

Anonymous

HABARI MBAYA Kwa Mashabiki wa ARSENAL Kuhusu Mchezaji Huyu Anayelipwa Pesa Nyingi Zaidi Klabuni Hapo!

Stori za kiungo wa kimataifa wa kijerumani mwenye asili ya kituruki Mesut Ozil kutaka kuihama klabu ya Arsenal zinazidi kuchukua nafasi katika magazeti mbalimbali ya michezo nchini Uingereza. Ozil anaripotiwa kuwa katika mipango ya klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. 

Stori zilizoandikwa september 24 ni kuwa, klabu ya Arsenal ipo katika mbio za kumshawishi Mesut Ozil aongeze mkataba mpya kabla ya usajili wa dirisha dogo kuanza. Mesut Ozil alijiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2013 akitokea klabu ya Real Madrid ya Hispania, kwa ada ya uhamisho wa rekodi wa klabu hiyo wa pound milioni 42.5.
36204

Mesut Ozil ambaye ana miaka 26 aliwahi kutamba katika vilabu vya Schalke 04Werder Bremen, Real Madrid na sasa anakitumikia kikosi cha Arsenal ila klabu hiyo ina hofu huenda kiungo huyo akatimkia klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Mesut Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika klabu ya Arsenal, analipwa pound 140000/= kwa wiki.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.