Thursday, September 24, 2015

Anonymous

TUMEJIPANGA! Wachezaji NGOMA, KAMUSOKO wa YANGA SC Wapewa Mipira ‘Iliyokufa’

DONALD NGOMA
Mshambuliaji Donald Ngoma.
Suleman Hassani, Pemba
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amewapa wachezaji wawili kazi ya kuhakikisha wanapiga mipira ya adhabu ndogo katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Simba.
Mipira hiyo ya adhabu maarufu kama ‘mipira iliyokufa’, itakuwa ikipigwa na kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma.
kamusoko
Kiungo Thabani Kamusoko.
Wachezaji hao walifanya kazi ya kupiga mipira hiyo katika mazoezi yaliyoongozwa na Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa kwenye Uwanja wa Gombani.
Mazoezi hayo yaliyofanyika juzi Jumatatu yalianza saa 9, Alasiri hadi Saa 12 jina kwenye uwanja huo, yalikuwa kivutio kwa mashabiki walioruhusiwa kuingia uwanjani hapo. 

Yanga ipo mjini hapa kujiandaa na mechi yake hiyo dhidi ya Simba na Pluijm alionekana kuwa makini kwa kila jambo linaloendelea huku akisisitiza lifanyike kwa ufasaha.
Tayari Tambwe, Ngoma na Kamusoko, kila mmoja ameshafunga katika mechi tatu za mwanzo wa Ligi Kuu Bara ambazo Yanga imecheza.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.