Friday, September 18, 2015

Anonymous

PICHAZ: RAIS KIKWETE AZINDUA JENGO LA KISASA JIJINI DAR


 Jengo la kisasa la mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umama-PSPF.
Rais Jakaya Kikwete amezindua jengo la kisasa la mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umama-PSPF- na kuyataka mashirika mengine nchni kujenga majengo ya kisasa ili kuleta imani na matumaini kwa wawekezaji kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, rais Kikwete licha ya kupongeza bodi ya wadhamini kwa kubuni wazo la kujenga jengo hilo,amesema jengo hilo limebadili mandhari ya jiji la Dar es Salaam na ni alama inayoweza kuvutia na kujenga matumaini kwa wawekezaji wanakuja nchini.
 Rais Jakaya Kikwete akizindua jengo la kisasa la mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umama-PSPF
Naibu waziri wa fedha Mhe. Adam Malima amesema ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji wa sera ya uwekezaji ambapo ameitaka PSPF kulitumia kama kitegeuchumi ambapo kutia halfa hiyo ameahidi serikali italipa madeni yote yanayodaiwa na mashirika ya hifadhi katika kipindi kifupi kijacho.
 
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamani wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umama-PSPF-Bwana George Yembesi amepongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuhamaisha uwekezaji uliohamasisha mfuko wa PSPF kubuni na kukamilisha jengo ambapo amesema moja ya changamoto kubwa inayoukabiri mfuko wa PSPF ni deni kubwa linaloidai serikali na kuitaka lilipwe kabla ya kukamilika kwa uongozi wa serikali ya awamu ya nne.
 
Majengo pacha ya  mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umama-PSPF-lina urefu wa mita 147 ni jengo refu la kwanza katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na ni jengo la nane kwa urefu katika bara la Afrika mpaka kukamilika limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 139.2.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.