Muigizaji wa tamthilia nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la Nana
Gichuru Jumanne hii alipoteza maisha kwa ajali mbaya ya gari baada ya
gari lake kugongana uso kwa uso na lori.
Polisi na mashuhuda walidai kuwa muigizaji huyo huenda alikuwa
akijaribu kuyapita magari kadhaa mbalimbali wakati akiwa kwenye gari
yake aina a BMW na ndipo alivaana na lori hilo lililokuwa likija mbele
yake.
Awali ya hapo, msichana huyo aliyewahi kufanya kazi Kenya Airways na
blogger anadaiwa kuandika vitu kwenye mitandao ya kijamii vilivyoonekana
kama alijitabiria umauti.
Katika post hizo mara nyingi amekuwa akiuliza kwanini watu huhoji uendeshaji wake wa gari.
“Life’s journey is not to arrive at the grave safely in a well
preserved body, but rather to skid in sideways, totally worn out,
shouting ‘HOLY CRAP!!!! WHAT A RIIIDEE,” aliandika Sept 11.
“To lace, red lips and oversized headphones and this amazing ride
#LifeAccessories #SetLife #HOLYCRAPWHATARIDE,” aliandika kwenye Instagram on September 10.
#LifeAccessories #SetLife #HOLYCRAPWHATARIDE,” aliandika kwenye Instagram on September 10.
Alikuwa muigizaji kwenye tamthilia ya ya Maisha Magic, “How To Find A Husband.”
Kwenye profile yake ya Instagram, Nana alijielezea kama ni: An
actor, writer, musician, voice artist, young filmmaker, entrepreneur,
travel junkie, maaard thinker and an unconventional human in Nairobi.
Chanzo: Capital FM

Note: Only a member of this blog may post a comment.