Mwimbaji wa muziki wa R&B, Jux amesema hawezi kufanya show za kampeni za kisiasa kwa kuogopa kuwachanganya mashabiki wake.
“Watanzania tulivyo, mimi kama kuna mtu ananipenda mpaka akaamua kuchora Jux au akaandika Jux kwenye mwili wake, mtu huyo nina nguvu ya kumshawishi na akafanya kitu bila ya yeye kutaka,” alisema.
Kwahiyo mimi naomba kama shabiki wangu uniangalia, mimi mwenyewe ni siri yangu, kuna kiongozi ambaye namuamini. Lakini wewe angalia mwenyewe, nenda Chadema au CCM. Msikilize Magufuli au Lowassa, wewe si una akili?”

Note: Only a member of this blog may post a comment.