Mwezi Mei mwaka huu, headlines zilikuwa Moscow baada ya mwanamke mmoja kunusurika kifo baada ya kujipiga risasi kichwani wakati akijipiga ‘selfie’ huku ameshikilia bastola mkononi.
Headlines zimehamia India, mtalii mmoja raia wa Japan amefariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka kutoka kwenye ngazi za jengo maarufu India Taj Mahal wakati akijipiga Selfie.
Polisi wamesema mtalii huyo baada ya kuanguka alipoteza fahamu na alifariki duniani wakati akitibiwa hospitali na alikua na mwenzake wakati wa tukio hilo ambaye amevunjika mguu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.