Johannesburg, Afrika Kusini
MAHAKAMA Kuu ya Rufaa nchini Afrika
Kusini, itasikiliza rufaa ya serikali dhidi ya mwanamichezo wa zamani
mlemavu, Oscar Pistorius, kuhusu hukumu dhidi yake Novemba 3 mwaka huu.
Tarehe 12 Septemba mwaka jana,
Pistorious alifutiwa mashitaka ya kuua kwa kukusudia na badala yake
akatiwa hatiani kwa kuhusika na kumpiga risasi na kumwua mpenzi wake wa
kike aliyekuwa mwanamitindo na mwanasheria, Reeva Steenkamp, usiku wa
kuamkia tarehe 14 Februari, 2013.
Pistorious alifyatua risasi nne kwenye
mlango wa maliwato uliokuwa umefungwa nyumbani kwake jijini Pretoria
Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) akifikiri ndani yake kulikuwa na
mpita njia aliyeingia humo.
Tarehe 21 Oktoba, Pistorius alihukumiwa
kifungo cha miaka mitano kwa kumwua Steenkamp, na miaka mitatu ya
kifungo cha nje kwa kuonyesha silaha hadharani katika mgahawa.
Mwezi ulipita Pistorius alikuwa
aachiliwe kutokana na kuonyesha tabia njema gerezani, lakini katika
dakika za mwisho Waziri wa Sheria na Misamaha ya Wafungwa, Michael
Masutha, aliamua kusimamisha uamuzi huo.
Hii ni kutokana na barua iliyotoka kwa
Umoja wa Harakati za Kupigania Haki za Wanawake wa Afrika Kusini
iliyopingwa kuachiwa kwa Pistorius.

Note: Only a member of this blog may post a comment.