Bibi akifurahia sera za Dk. Magufuli.
Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Pombe Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda mkoani Geita leo.
Umati wa watu katika mkutano wa kampeni Runzewe.
Dk. Magufuli akiwapungia mkono wananchi Miji ya Buselesele na Katoro.
Msafara wa Magufuli kelekea katika mkutano wa kampeni katika Mji mdogo wa Katoro.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Musukuma akihutubia kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli mjini Katoro.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Jonh Pombe Magufuli, leo alifanikiwa
kuingia Mkoa wa Geita baada kumaliza kampeni zake mkoani Kagera.
Miongoni mwa maeneo aliyofanya mikutano
hiyo leo ni pamoja na Vijiji vya Lulenge, Bukililo, Bugalama, Magamba,
Mluzagamba, Nyakaula, Lunzewe vyote vya wiloayani Ngara mkoani Kagera.
Baada ya kuingia mkoani Geita, Dk
Magufuli alifanya mikutano ya kampeni Vijiji vya Bwanga, Buselesele,
Katoro na kumalizia Geita Mjini.
Dk Magufuli aliwaahidi wakazi wa Geita
na Katoro kuwa, endapo watamchagua kuwa rais wa Tanzania, ataondoa kero
za wakazi hao kufukuzwa maeneo ya migodi, kuboresha miundombinu na
utendaji wa migodini, kuweka utaratibu utakawawezesha wachimbaji
wadogowadogo kunufaika na migodi hiyo, kuondoa kero za maji, kuongeza
barabara za lami sehemu mbalimbali alizopita na kutoa elimu bure kuanzia
darasa la kwaza mpata kidato cha nne.
Kesho alhamisi, Magufuli anatarajiwa kuelekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuwania urais wa Tanzania.
PICHA NA STORI: RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO GEITA

Note: Only a member of this blog may post a comment.