Polisi ambaye ni mstaafu kwa sasa amedai kuwa Tupac Shakur anaweza kuwa bado yupo hai.
David Myers, ambaye kwa sasa yupo mahtuti hospitali amedai kuwa
alilipwa dola milioni 1.5 kumsaidia rapper huyo kudanganya kifo chake
mwenyewe. 2Pac alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi mwaka 1996
alipokuwa na umri wa miaka 25.
Lakini sasa Myers anasema anataka ulimwengu ujue ukweli kutoka kwenye
kitanda chake anakokaribia kufia. “Ulimwengu unahitaji kujua
nilichokifanya. Ninaona aibu kuwa niliacha fedha iathiri maneno yangu,
na siwezi kufa bila ulimwengu kujua.”
Anadai kuwa Suge Knight ambaye kwa sasa yupo jela akisubiri hukumu ya
mauaji alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye mipango hiyo. Watu zaidi ya
30 walidaiwa kulipwa kusaidia kudanganya kifo hicho wakiwemo polisi,
madaktari na mashuhuda.
September 7, 1996, Shakur alipigwa risasi kadhaa akiwa barabarani
huko Las Vegas, Nevada. Alikuwa kwenye pambano la ngumi kati ya Mike
Tyson na Bruce Sheldon.
CHANZO: MIRROR.CO.UK

Note: Only a member of this blog may post a comment.