Muigizaji maarufu Bongo, Musa Yusuf ‘Kitale au Mkude Simba’.
Gladness Mallya na Hamida Hassan
SIASA zitawatoa
roho mastaa! Waigizaji maarufu Bongo, Musa Yusuf ‘Kitale au Mkude
Simba’ na Jimmy Mafufu wamejikuta wakitukanana chanzo cha yote kikitajwa
kuwa ni mambo ya siasa.
Mtoa habari aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya Ijumaa
kwamba, mwanzo wa uhasama wao ni baada ya Mafufu kumuunganisha Kitale
na Ukawa kama mmoja wa wasanii wanaounga mkono umoja huo lakini baadaye
Kitale akarudi kumuunga mkono mgombea kutoka CCM, Mhe. John Magufuli.
“Unajua Kitale alijua kuwa kule Ukawa
msanii akienda anapewa mpunga, sasa alipoona mambo siyo mambo,
akajirudia zake kwenye chama la nyumbani (CCM) ndipo bifu lilipoanzia.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Kitale na kumsomea madai hayo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Achana na huyo Mafufu sitaki
kumzungumzia naona anatafuta umaarufu, kila mtu ana uhuru wa kuwa chama
anachokitaka, nimwambie tu siasa zitapita na maisha yataendelea kama
kawaida, mwache aendelee kuongea.”
Kwa upande wa Mafufu alipotafutwa
alisema: “Kitale ni mjinga alikuja kuniomba nimuunganishe na Lowassa,
nikafanya hivyo baada ya kuja alidhani kuna hela akaamua kuondoka.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.