Imelda Mtema
DHARAU! Meneja wa mcheza filamu
Wema Sepetu, Martin Kadinda ambaye pia ni mwanamitindo, katika hali
isiyo ya kawaida, amemdhalilisha rafiki kipenzi wa zamani wa bosi wake
huyo, Kajala Masanja kwa kumwelezea kuwa historia za maisha yao ni
tofauti mno, kitu kinachotoa picha kuwa urafiki wao usingeweza kudumu.
Akizungumza na gazeti hili hivi
karibuni, Kadinda alisema makuzi ya mastaa hao wawili kuanzia shule na
aina ya maisha ni vitu viwili tofauti na hawaendani, kwani hata urafiki
wao haukutoka moyoni, bali ulisukumwa na upendo wa mtoto wa Kajala kwa
Wema.
“Kajala kasoma uswahilini na Wema kama
unavyojua, kapata elimu yake ya uhakika kwenye shule za maana, hata
maisha yao ya kawaida unaona yana tofauti kubwa, kama siyo Paula (mtoto
wa Kajala) kumpenda Wema, wawili hawa wasingeweza kuwa marafiki,”
alisema Kadinda.
Gazeti hili lilimtafuta Kajala ili
kuzungumzia maneno hayo ambapo alionyesha kusikitishwa kwake na kauli
hiyo, akidai kwa kipindi chote wao wakiwa marafiki, hakuwahi kuona
Kadinda akitilia shaka urafiki wao.
“Daah mimi hata nashindwa nizungumzeje,
simuelewi kabisa huyo meneja maana yeye huko nyuma sikuwahi kusikia
akisema hivyo, amenishangaza sana na bado nitaendelea kumshangaa,”
alisema Kajala.
Kadinda alitoa kauli hiyo alipotakiwa
kuzungumzia urafiki wa bosi wake na staa mwingine wa filamu, Yobnesh
Yusuf ‘Batuli’ kwani historia inaonyesha Wema hadumu na marafiki.
“Ki ukweli kabisa urafiki wa Wema na
Batuli mimi naukubali kwa asilimia zote kabisa, kwa kuwa Batuli anapenda
kufanya mambo yake ‘private’ na maisha hayo ndiyo staa anapaswa
kuyaishi, kuliko kuyaanika kila wakati maana watu lazima wakuchoke”
alisema Kadinda.

Note: Only a member of this blog may post a comment.