Siku chache baada ya Taasisi ya TWAWEZA
kutoa Ripoti ya Utafiti waliofanya kuelekea Uchaguzi Mkuu Tanzania,
October 25 2015… Viongozi wa Vyama mbalimbali wametoa misimamo yao
kuhusu Utafiti huo.
Jana September 23 2015 January Makamba alitoa Taarifa kuhusu msimamo wa CCM kwenye Utafiti huo, ninakusogezea na hii pia mtu wangu, Taarifa kutoka Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo, Nickson Tugala alitoa taarifa hiyo >>> “Chama
cha ACT kimeyapokea na kuyapitia Matokeo ya utafiti uliofanywa na
TWAWEZA… Utafiti unaonesha Ilani ya ACT imezingatia mahitaji ya
Watanzania“>>>
“ACT
tunafarijika kwamba Chama chetu ni Chama pekee nje ya CCM na UKAWA
kilichotajwa na Wapigakura zaidi ya Asilimia moja, kimekuwa chama cha
nne katika kukubalika kwa Wapigakura nyuma ya CCM CHADEMA na CUF” >>> Nickson Tugala.
“Takwimu
hizo zilikusanywa wakati ambao ACT-Wazalendo hakijamtangaza Mgombea
wake wa Urais wala tulikuwa hatujafanya Uzinduzi wa Kampeni… Kama
Utafiti huu ukirudiwa tunaamini tutafanya vizuri zaidi” >>> Nickson Tugala.
Sauti yenye Taarifa yote hii hapa chini mtu wangu, Ripoti kutoka Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Dar es Salaam.

Note: Only a member of this blog may post a comment.