“Naomba mniombee, Mniombee kwelikweli, nyie walutheri mnasababu ya kuomba zaidi. Kwa sababu nchi hii tangu iumbwe haijawahi kupata mlutheri kuwa rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa alikuwa Mkatoliki, sasa nadhani Mungu anatuongoza vyema. Kwa hiyo naomba mniombee sana,” Lowassa anawaambia waumini wa kanisa hilo.
Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba amepost kipande hicho cha video kwenye Twitter na kueleza jinsi alivyoshangazwa na maelezo ya Lowassa.“Lowassa tells a Lutheran congregation that country needs a Lutheran President. Politics aside, how dangerous is this?” Alitweet January Makamba.

Note: Only a member of this blog may post a comment.