Wednesday, September 9, 2015

Anonymous

BASATA Ladai Adhabu Kwa SHILOLE Ipo Pale Pale...Ushahidi Unakusanywa Kumtwanga Nyundo Nyingine Kali Zaidi!

11849422_614272212008606_1194790121_n
Shilole anaweza akawa anafurahia bata za Marekani baada ya kutumbuiza kwenye show nchini humo, lakini bado BASATA haijamalizana naye.
Katibu Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa, BASATA, Geofrey Mngereza ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa. 

Mngereza alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa Shilole imetokana na sheria na kanuni zilizotokana na bunge na kwamba kwa sasa wanakusanya ushahidi ili kuchukua hatua.
“Litachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosema,” alisema Mngereza.
“Kwahiyo itapitia process ile ile ambayo imetumika hapo awali kuweza kutoa adhabu. Kwahiyo ni kitu ambacho kinafanyiwa kazi.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.