Thursday, September 3, 2015

Anonymous

BABU SEYA,PAPII VICHEKO GEREZANI

SIKU chache baada ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kueleza kuwa atawatoa gerezani wanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wanaotumikia vifungo vya maisha jela kwa kosa la kuwanajisi watoto tisa, imeelezwa kuwa wawili hao wamepata furaha na kuchekelea hivyo kuwa na matumaini mapya.

Vyanzo vyetu ndani ya Gereza la Ukonga wanamotumikia vifungo vyao zinasema wafungwa hao baada ya kusikia habari hiyo, siku hizi wamekuwa wafuatiliaji wazuri wa habari zinazoandikwa magazetini.

“Siku ile Lowassa alipotoa tamko Viwanja vya Jangwani, Babu Seya na Papii walifurahi sana, waliliona tumaini jipya,” alisema mtoa habari huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalum.Mwanasheria mmoja, Dk. Ngali Maita alipoulizwa maono yake juu ya kauli ya Lowassa alisema: “Inawezekana akiwa rais wa nchi akawasamehe kwa sababu katiba inamruhusu.

“Ibara ya 45: 1 (a) inasema rais anaweza kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote na anaweza kutoa msamaha huo ama bila masharti au kwa masharti kwa mujibu wa sheria.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.