Friday, September 4, 2015

Anonymous

AJALI: MSANII MAARUFU KINGWENDU ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI MBAYA YA GARI WAKATI WA KAMPENI

Mwigizaji maarufu, Kingwendu amenusurika kifo baada ya ajali mbaya ya gari iliyotokea leo Wilayani Kisarawe.
Kingwendu amekumbana na ajali hiyo akiwa katika kampeni zake za kuwania ubunge katika Jimbo la Kisarawe.
Mwigizaji huyo anawania nafasi hiyo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na kampeni zake zimekuwa zikipamba moto.

Msemaji wa Kingwendu, Msanii mwingine, King Sapeto amesema aliyeumia ni mtu mmoja tu aliyeumia anajulikana kwa jina la Big.
“Big ndiye pekee aliyepata majeraha,” alisema King Sapeto bila ya kutoa maelezo zaidi.




KING SAPETO (KUSHOTO) AKIWA NA KINGWENDU KATIKA MOJA YA KAMPENI.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.