Dr
Magufuli ameongeza kuwa yeye si mwanasiasa mzuri bali ni mtendaji zaidi
na kwamba baraza la mawaziri atakaloliunda litakuwa ni baraza la
mawaziri la kuwatumikia wananchi kwa kutatua kero zao hasa wale wa hali
ya chini na kuwataka watakaoteuliwa katika baraza lake wajipange.
Katika
mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na mwenyekiti wa chama hicho taifa
Mh Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania kuwa hawatajuta
kumchagua Dr Magufuli kuwa rais wa awamu ya tano kwa kuwa ni mwadilifu
na mzalendo na kwa kuchaguliwa kwa Dr Magufuli yeye rais Kikwete atapata
usingizi mwema.
Dr
Magufuli amefanya pia mikutano katika maeneo ya Ruaha, Mikumi, Kilosa
na kisha Morogoro mjini ambapo baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi
wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo mwenyekiti wa
Chadema wilaya ya Kilosa Bwana Selemani Simba, katibu wa Chadema wilaya
ya Kilosa Ibrahimu Selemani na katibu wa jimbo kilosa kati Bwana Musa
Ngongi.
Mchakamchaka
wa kampeni za uraisi zikizidi kupamba moto, leo hii Mgombea wa nafasi
ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM Ndugu John
Makufuli ametia tim Manispaa ya Morogoro.
Akiwahutubia
maelfu waliofurika katika uwanja wa Jamhuri, Ndugu Magufuli ameahidi
kushughulikia tatizo la ajira kwa kuhakikisha anafufua viwanda
vilivyokufa ili kuhakikisha wakazi wa Morogoro wanapata ajira.
Aidha
Mh: Magufuli maarufu tingatinga, amesema katika uongozi wake
atahakikisha anawashughilikia wala rushwa hasa mapapa ya rushwa ili
kuhakikisha anaiweka Tanzania yenye usawa.
Mgombea Ubunge Morogoro Mjini ndugu Azizi Abood
Mzee Yusuph Makamba
Mgombea
urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amesema serikali yake itatilia
mkazo suala la ukusanyaji wa kodi hasa kwa wawekezaji wa nje pamoja na
kuangalia upya misamaha ya kodi ili kuiwezesha serikali kukusanya fedha
nyingi zitakazosaidia kutoa huduma za kijamii kwa ajili ya maendeleo ya
watanzania.
Dr
John Pombe Magufuli ameyasema hayo katika uwanja wa amhuri uliopo
mkoani Morogoro wakati akinadi sera zake kwa mamia kwa makumi ya
wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo amempongeza rais Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuongeza mapato ya serikali na kuongeza kuwa serikali yake
itaongeza mapato ya serikali kwa kuangalia upya suala misamaha ya kodi
kwa wawekezaji hususani wa kigeni.
Sehemu ya wakazi wa Morogoro
Rais Jakaya Kikwete

Ndugu John Magufuli
Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Innocennt Karogeres
Maelfu ya wakazi wakimsikiliza Magufuli
Nukuu:
Mzee
Makamba "Lowassa alitaka kuondoka CCM tangu 1995, Nikamsihi,
alishakataliwa kutokana na ufisadi wake. Namuomba kwenye mdahalo,
tuliushangaa utajiri wake akiwa mdogo, Hatufai"
Innocent -" TunakuombMagufuli ukawafunge mafisadi na waliopora ardhi"
Kikwete- " Magufuli anatosha"

Note: Only a member of this blog may post a comment.