Nuh Mziwanda ana wakati mgumu wiki hii. Wema Sepetu na Idris Sultan
wamemharibia siku yake na kama haitoshi, Linex naye yupo shingoni mwake!
Muimbaji huyo wa Salima, ametumia mtandao wa Facebook kumtupia dongo
‘Mzee wa Vipepeo’ kwa kukejeli uamuzi wake wa kujichora tattoo yenye
jina la Shilole.
“Hao wanawake zenu mnao wachora tattoo za majina yao si pia walikua
wanawake zetu tukashindwa tabia zao so jiandae kufuta tattoo yako,”
aliandika Linex.
Nuh amejichora tattoo mbili zenye jina la mpenzi wake huyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.