Saturday, August 1, 2015

Anonymous

Video ya Christian Bella haipigwi nje, karidhika? Belle9 anajutia kujitoa mitandaoni? Kauli ya BASATA kwa Shilole… #255 July31

Unajua kwa nini Video ya ‘Nashindwa’ ya Christian Bella haipigwi nje? mwenyewe amesema kuna sehemu ambayo haikuwa inatakiwa ndani ya video yake hiyo ndio sababu inayochangia kutoonyeshwa..hakuona sababu ya kuibadilisha, anashukuru kuona inapigwa sana kwenye televisheni za hapa nyumbani.

Christian Bella
‘Sumu ya Penzi’ ya Belle 9 imetoka…mwenyewe anasema baada ya kupata mtu wa kumsimamia akaamua kuziweka kwenye albamu na kutoka huku nyingine zikiwa hazijatoka…pia amesema anajutia kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu wengi walilalamika na wengine kumtukana…pia amesema imemsaidia kuwa karibu na mtoto wake mdogo ambaye kwa sasa analea.

Belle9
Baada ya BASATA kumfungia Shilole kutokana na picha zilizosambaa mitandaoni akiwa anafanya shoo Ubelgiji..leo mwenyewe kafunguka na kusema ameonewa na si haki kufanyiwa hivyo licha ya yeye kuomba msamaha na kusamehewa kabisa…BASATA nao wamezungumza na kusema kifungo chake kitakuwa fundisho…pia anaweza kwenda kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana kama anaona hajatendewa haki.

Shilole
Wasikilize hapa..

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.