Wednesday, August 5, 2015

Anonymous

USAJILI VPL: MAVUGO Afunguka Kuhusu YANGA SC

1434210602_laudit_mavugo.jpgMshambuliaji hatari raia wa Burundi anayekipiga Klabu ya Vital’O, Laudit Mavugo.
Mohammed Mdose, Dar es Salaam
KUFUATIA kuzagaa kwa taarifa za Yanga kutaka kuwazidi kete wapinzani wao Simba, kwa kumsajili mshambuliaji hatari raia wa Burundi anayekipiga Klabu ya Vital’O, Laudit Mavugo, mwenyewe ameibuka na kusema kuwa ni kweli Yanga wanamnyemelea na tayari taarifa zimeshamfikia akiwa huko Burundi.

Hivi karibuni, Simba walipigania kumnasa mchezaji huyo, lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya uongozi wa pande zote mbili kutoafikiana baadhi ya masharti, kubwa likiwa dau la kumnyakua. Vital’O walitaka wapewe dola 100,000 (zaidi ya shilingi milioni 200), hapo ndipo Simba waliposhindwa.

Akizungumza na Championi Jumatano moja kwa moja kutoka Bujumbura, Burundi, mshambuliaji huyo anayesifika kwa kulijua lango vilivyo, alisema kuwa taarifa za kutakiwa na Yanga ameshazipata, hivyo akawaambia kama wanaihitaji huduma yake, basi wamfuate na kukaa mezani kuzungumza.

“Taarifa za Yanga kunitaka nimezisikia tu juu kwa juu kama unavyozisikia wewe ndugu yangu, lakini bado hawajanifuata rasmi kuongea na mimi ingawa ni kweli wananitaka. Kama kutakuwa na maelewano mazuri nitakuja kucheza soka huko Tanzania, hakuna tatizo katika hilo,” alisema Mavugo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.