Namba ya siku Pedro atakazoendelea kukaa ndani ya klabu ya FC
Barcelona zinahesabika baada ya Rafinha kupewa nafasi ya kuanza katika
kikosi cha kwanza kinachocheza na Sevilla katika Spanish Supercup.
Pedro mwenye asili ya visiwa vya
Canary, amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United, na usiku
wa leo kocha Luis Enrique alimuweka benchi huku mkurugenzi wa michezo wa
timu hiyo Robert Fernandez amekiambia kituo cha Esport 3 kwamba Pedro
ameomba kuhama.
“Pedro amenitaarifu rasmi kwamba
anataka kuondoka, ila kwa sasa bado hatujapata ofa. Ikiwa kuna klabu
inayomtaka basi itabidi walipe fedha ya kuweza kuvunja mkataba wake
ambayo ni £21m.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.