Hamida Hassan
Wapo ambao wanapo jaaliwa kupata watoto, hupenda wafuate nyayo zao. Kuna wanamuziki, wanasoka, wanasiasa, waigizaji na watu wa fani nyingine ambao wamewavalisha watoto wao viatu vyao.
Hawa waliandaliwa na wazazi wao kuingia kwenye siasa na wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hatua ya uwaziri, ubunge ndiyo muelekeo mzuri wa kuja kuwa marais na nguvu zao ni kutokana na jinsi walivyoandaliwa.
Kibongobongo wapo mastaa ambao wanawaandaa watoto wao wawe mastaa wa kesho. Hilo linaonekana kutokana na jinsi wanavyowaweka na wengine kufikia hatua ya kuwaingiza kwenye fani zao wakiwa na umri huo mdogo.
Kutokana na hilo, leo nitakupa orodha ya watoto wa mastaa ambao kuna kila dalili kuwa wazazi wao wanawaandaa kuwa mastaa wa kesho.
Patrick Peter
Huyu ni mtoto wa staa wa filamu, Rose Alfonce ‘Muna’. Mtoto huyo amekuwa akishirikishwa kwenye filamu mbalimbali.
Aidha, maandalizi yake na muonekano wake kuanzia mavazi, mikato ya nywele na swaga zake kwa ujumla zinaashiria moja kwa moja kuwa atakuja kuwa staa mkubwa.
Huwezi kuamini lakini mtoto huyo amefunguliwa hadi akaunti ya Instagram anayoiendesha mwenyewe.
Tanzanite Hamis Baba
Huyu ni mtoto wa Hamis Baba ‘H-Baba’ na Flora Mvungi. Kabinti haka kamekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali kutokana na wazazi wake wanavyokaweka.
Amekaa kistaa, anavaa kistaa na hata staili ya nywele zake mara nyingi huwa kama zile za akina Amber Rose (Zinakuwa fupi kisha zinapakwa rangi).
Kuashiria kuwa mtoto huyu anaandaliwa kuwa mwanamuziki mkubwa wa baadaye, baba yake amekuwa akimfundisha kupiga kinanda na amefunguliwa akaunti ya Instagram.
Paula Paul Matthysse
Nani asiyemjua mtoto huyo pichani juu? Ni mtoto wa Kajala Masanja na Paul Matthysse ‘P-Funk’. Huyu anakwenda kwa kasi sana kuelekea kwenye ustaa kama wazazi wake.
Anajichanganya kwenye maeneo mbalimbali ya burudani, mavazi yake na hata anavyojiweka anaonesha wazi kuwa, kesho yake itashikwa na ustaa.
Sonia Tyson
Ni mtoto wa msanii wa filamu Yvonn Sherly ‘Monalisa’ na marehemu George Tyson. Ameandaliwa kisanii kwa kuingizwa kwenye matangazo mbalimbali. Enzi za uhai wa baba yake aliwahi kusema kuwa, mwanaye huyo ana kipaji na kuna uwezekano mkubwa akawa muigizaji mkubwa siku za baadaye.
Russell ‘Juju’
Huyu ni mtoto wa kwanza wa Zamaradi Mketema. Muonekano wake umekuwa ukifurahisha na mtu hutamani kuona picha zake na jinsi anavyovalishwa. Ana vituko sana na ile staili yake ya kiduku ambayo hupenda kunyolewa ndiyo huwafanya wengi waamini anaandaliwa maisha ya kistaa.
Hao ni baadhi ya watoto wa mastaa ambao ukiwafuatilia sana utagundua wazazi wao wanawaandaa kuwa mastaa wa baadaye huku wengine wakiwa tayari wameshaonesha vipaji vyao.
Si unakumbuka staa wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikoanzia? Alianza kuigiza akiwa mdogo sana. Sasa unashindwa nini kuamini kuwa, Patrick Peter atakuja kuwa staa wa kuziba nafasi za akina marehemu Steven Kanumba?

Note: Only a member of this blog may post a comment.