Imelda mtema
Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat amefunguka kuwa hakuna kitu kibaya kama mkorogo kwa kuwa yeye anautumia lakini anajua madhara yake ni makubwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Nyoshi alisema kuwa kama kuna ambaye hajawahi kutumia mkorogo basi asitumie kwa vile ni hatari na pia unamaliza pesa sana maana siku ukiukosa kama hwwuna hela utatamani kuiba.
“Jamani mimi nilihamasika kutumia mkorogo kupitia baba yangu, alikuwa akinipa moyo kuwa nitaonekana vizuri lakini sasa naona madhara yake, wanaotamani kujichubua siwashauri maana watakuja kujuta,” alisema Nyoshi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.