Monday, August 24, 2015

Anonymous

THEA APATA MWANAUME WA KUMLEA


Ndicho alichokitaka! Kwa taarifa yako, mwigizaji ‘lejendari’ Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ juzikati alifunguka kuwa kwa sasa amepata mwanaume anayejua kumlea na kumtunza ambapo anatarajia kumuweka wazi muda si mrefu.

Mwigizaji ‘lejendari’ Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
Akistorisha na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita ndani ya Hoteli ya Protea jijini Dar, Thea alisema kuwa baada ya kuachana na aliyekuwa mumewe Michael Sangu ‘Mike’ na kukaa bila kuweka wazi ‘anabanjuka’ na nani, sasa anatamba kumpata mwanaume anayejua thamani ya mwanamke.
“Nitamuweka wazi ‘soon’ shemeji yenu ili mumjue kwani nimeshamchunguza na kugundua kuwa ananifaa na nitakuwa naye katika safari ya mapenzi,” alisema Thea.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.