Msanii wa kike mwenye vituko Tausi Mdegela ‘Miss Iringa’ anasema kuwa hakuna mtu muhimu sana katika maisha yake ya sanaa kama msanii nyota katika vichekesho King Majuto, kwani bila mchekeshaji huyo hakuna mtu yoyote angemjua kupitia sanaa.
“Mimi bwana Mzee King Majuto ni baba yangu haswa, maana bila yeye hata wewe usingenijua nilikuwa kila nikiomba watu nionyeshe kipaji changu cha uigizaji wanakataa kunisapoti, lakini nilipokutana na Mzee Majuto hakuninyanyapaa,”anasema Tausi.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anasemamiwa na muongozaji wa filamu nchini Lamata kama meneja wake anasema kuwa pamoja na muonekano wake kuwa ni mdogo lakini ana uwezo mkubwa sana katika kuigiza na kumfanya aigie katika kundi la wasanii wanaotamba katika uchekeshaji kwa wanawake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.