Friday, August 7, 2015

Anonymous

TANESCO Hii ni Dharau Kubwa Sana Kwa Wananchi! Serikali Iko Wapi?!

Ni takribani mwezi sasa, kumekuwa na tabia fulani hivi ambayo TANESCO wanaiendekeza na Serikali kufumbia macho hili wakati mwananchi akiteseka. Maisha yamekuwa ya kuviziana hasa kwa ajili ya umeme. Yaani unaishi kwa 'tension' hujui umeme utakatwa saa ngapi na utarudi saa ngapi. Nimetembelea mikoa ya Mwanza, Morogoro, Shinyanga, Geita, n.k hali ni hiyo hiyo.

Uzalishaji mwingi(kimapato) wa mwananchi wategemea umeme, wengi kwa ajili ya biashara ndogo ndogo mf. Mashine za kusaga, kuchomelea, saluni, n.k lakini hata katika nyumba za kulala wageni, hoteli ingawa wanatumia nguvu nyingine ya umeme(generator) bado ninaamini ni stahili yao kujua;

1. Shida ni nini (kwanini umeme ukatike namna hii)?
2. Kama kuna 'mgao wa umeme' ni kwanini wananchi wasijulishwe?
3. Hii hali itaendelea kuwepo hadi lini?

Kwa nchi yenye vyanzo vingi vya umeme (maporomoko,makaa ya mawe,vyura wa kihansi, n.k) ni aibu hali kuwa namna hii lakini zaidi ya yote, ni vyema taarifa kutolewa mapema mtu kujua ratiba na kujiandaa vilivyo/kujipanga.

Kama wewe ni mtanzania na umeguswa na hili suala tafadhali usikae kimya toa maoni yako na share na wenzako habari hii!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.