Brighton Masalu
ELIZABETH Michael
‘Lulu’ na aliyekuwa mume wa muimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha,
Emmanuel Mbasha wamezua gumzo, minong’ono na maswali mengi kufuatia
kutumia muda mwingi kukaa kwa ukaribu zaidi na kwa mapozi
tofautitofauti.
Tukio la wawili hao kugandana mithili ya
ruba, lilijiri hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga
jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa Albamu ya Tunapendwa na Mungu ya
muimbaji Boniface Mwaitege na kuzua hisia za huenda ‘wanabadilishana
joto’.
“Mmh, hawa mbona wako ‘beneti’ kiasi
hicho? Halafu ona wanavyooneshana mahaba jamani, kuna kitu hapo, siyo
bure,” alisikika mdau mmoja wakati akijadiliana na wenzake.
Hata hivyo, mwanahabari wetu alimuuliza Mbasha juu ya ukaribu wao ambapo alijibu kwa kifupi kuwa ni upendo wa kawaida tu.
“Aah, kaka mbona ni kawaida tu, upendo wa Agape (kawaida), hakuna cha ziada kati yangu na Lulu,” alisema Mbasha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.