Staa wa muziki na filamu Selena Gomez.
Hollywood, marekaniStaa wa muziki na filamu Selena Gomez amedai kuwa hajutii kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Justin Bieber kwa sababu anaamini kuwa naye ilikuwa ni sehemu ya tuisheni ya kujifunza mapenzi.
“Bado sina mpenzi lakini naamini penzi langu lijalo litakuwa zuri na la kipekee sana kwangu kwa sababu nimejifunza mengi kupitia uhusiano wangu na Bieber. Wala sijutii kuachana naye,” alisema Selena ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka na ‘muuza sura’ anayejulikana kwa jina la Nick Jonas huku Justin Bieber akitoka na msichana anayefahamika kwa jina la Jayde Pierce.

Note: Only a member of this blog may post a comment.