Wednesday, August 19, 2015

Anonymous

PICHAZ: JOKATE Habanduki kwa KIBA, Amfuata Kenya, Ashuhudia Wakirekodi na Sauti Sol

Jokate Mwegelo hatoki begani mwa mahabuba wake, Alikiba.

Wawili hao wapo jijini Nairobi, ambapo Kiba yupo kurekodi kipindi cha Coke Studio na Jokate ameamua kuungana naye kumsaidia kumpunguzia baridi la jiji hilo ambalo kipindi hiki linadaiwa kuwa katika kilele chake.
Jokate ameshare picha kadhaa kwenye Instagram zikimuonesha akiwa na hitmaker huyo wa Mwana na pia kumshuhudia mwandani wake huyo akirekodi wimbo anaofanya na kundi Kenya, Sauti Sol.

Hata hivyo huenda Jokate akawa ameenda pia kufanya kazi zake binafsi kwakuwa katika picha moja anaonekana akiwa na mtangazaji mrembo wa TV wa nchini humo, Sarah Hassan.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.