Ukiachilia mbali Diamond Platnumz wa Tanzania na rapper AKA wa Afrika
Kusini, Davido ni staa mwingine wa Afrika aliyepata mtoto hivi karibuni
na anajivunia kuwa BABA.
Davido ambaye ni miezi mitatu imepita toka apate mtoto wa kike,
amekuwa akishare na followers wake picha za mwanaye, ikiashiria kuwa ni
jinsi gani uwepo wa mtoto huyo duniani unamuongezea furaha iliyoshindwa
kukamilishwa na mali/mkwanja anaoumiliki kutokana na kazi yake ya muziki
pamoja na utajiri wa wazazi wake.
Wakati Diamond na Zari bado hawajataka kuionesha sura ya mtoto wao
Tiffah, Davido ameshare picha mpya Instagram inayomuonesha vizuri sura
ya mtoto wake. Picha hiyo ilisindikizwa na maneno: “GETTIN TOO BIG”.

Note: Only a member of this blog may post a comment.